Ugomvi wa Gwajima na Makonda Wamfikia Askofu Mkuu wa KKKT..Ajiingiza na Kuibuka na Hoja Hizi Kuntu..!

Sakata la Gwajima na jina la Daudi Bashite limeendelea kutikisa maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo Askofu  (mstaafu)  wa kanisa la  kiinjili la  Kilutheri  Tanzania (KKKT)  dayosisi ya  Iringa Dkt. Owdenburg Mdegella amefunguka  na kuwataka wananchi kujikita katika shughuli za  kiuchumi badala ya kupoteza muda  mwingi  kujadili  mambo  ya  Daud Bashite.



Askofu Mdegella alisema hayo wakati  akitoa  salama  za Pasaka  jana katika  usharika  wa kanisa kuu, ambapo alidai kuwa watanzania wanapoteza  muda  mwingi kwa jambo hilo badala ya  kushughulika na mambo ya msingi yenye  tija kwa  Taifa .

Alisema kwa wiki tatu watu wanajadili Bashite na Gwajima badala ya kufanya kazi kwa kuwa Gwajima na Bashite wote wametoka Mwanza hivyo wanajuana vizuri.
Alisistiza kama kuna mtu  amedandia  vyeti  atakamatwa  kwa  utaratibu   na kuwataka watu wengine kujikita katika kufanya kazi


EmoticonEmoticon