Mavoko: Nimeamua Kuja na Mtindo wa Kuimba Utakaokuwa Wangu Peke Yangu

Rich Mavoko amesema anaendelea kutengeneza mtindo wa kuimba utakaomfanya asifanane na msanii yeyote.

Ameiambia Bongo5 kuwa mtindo huo aliuanzisha kama majaribio kwenye Kokoro na baada ya kuona watu wameuelewa, ameuboresha zaidi kwenye wimbo mpya aliofanya na Harmonize, Show Me.

 “Nilikuwa natamani nipate style ambayo haifanywi na watu wengine Bongo, kama nilivyofanya kwenye Kokoro na kwenye verse ya Show Me,” Mavoko ameiambia Bongo5. “Soko pia linahitaji ubunifu, hata ninachokifanya ni sehemu ya ubunifu sababu nimejaribu kubadilika,” ameongeza muimbaji huyo huku akielezea kuwa ngoma zijazo zitadhihirisha zaidi anachokisema.

Kuhusu wimbo Show Me, Mavoko amesema yeye alianza kuwa na wazo na kisha kumshirikisha Harmonize aliyetengeneza msingi.

 “Sababu mimi ndiye nilikuwa nina wazo, picha nzima nilikuwa naijua Harmonize alivyoanza verse ya kwanza alinifungua baadhi ya vitu kwamba mimi ntafanya hivi, na wewe utafanya vile.” 


EmoticonEmoticon