SERIKALI Yakwama Upelelezi kesi ya Wema Sepetu

Leo April 12, Msanii Wema Sepetu alifika katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam kusikiliza kesi ya tuhuma za kutumia na kukutwa na Dawa za kulevya, ambapo UPANDE wa Jamhuri umeshindwa kukamilisha upelelezi dhidi ya kesi inayomkabili msanii huyo.

Upande wa Mashtaka uliowakilishwa na wakili wa Serikali Constantine Kakula, ulidai kuwa kesi hiyo imefika kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi haujakamilika hivyo ipangiwe siku nyingine.

Hakimu  Mkazi Mkuu Thomas Simba, ameuhoji upande wa Jamhuri, kutokana na kuchelewesha upelelezi wa kesi hiyo ambapo kila tarehe inayotajwa Serikali inadai kuwa upelelezi haujakamilika.

Kesi hiyo imeahirishwa na itatajwa tena tarehe 2 mwezi Mei mwaka huu.


EmoticonEmoticon