WEMA Sepetu Afungukia Ushirikina Unaodaiwa Kutokea Nyumbani Kwake

Image result for WEMA Sepetu

Mkali wa Bongo Muvi, Wema Isaac Sepetu amefungukia ushirikina unaodaiwa kutokea nyumbani kwake, Ununio jijini Dar, baada ya kuenea kwa habari zilizomhusu mwanamke mzee ambaye hakujulikana mara moja aliyedaiwa kudondoka na ungo getini kwa mrembo huyo.

Chanzo chetu ambacho kilidai kuwa na picha za tukio hilo lililomuonesha mzee huyo akiwa amezingirwa na watu wakimuhoji, kilidai kuwa, mwanamke huyo alidondoka getini hapo na ungo mchana kweupe, ishu ambayo ilivuta hisia za watu wengi waliojaa getini kwa staa huyo wakati mwenyewe akiwa hayupo.

“Yaani pale Ununio kulifurika kwa sababu watu walijazana baada ya mwanamke huyo kuanguka na ungo pale.

“Inavyoonekana Wema siyo wa mchezomchezo kabisa maana kama alitumwa kumfanyia ubaya, amefeli kabisa,” kilisema chanzo hicho.

Akizungumza na Wikienda katika mahojiano maalum juu ya sakata hilo, Wema alishangazwa na habari hizo na kusema kuwa, hakuna kitu kama hicho kimewahi kutokea nyumbani kwake.

“Jamani mimi niko kambini, narekodi filamu yangu, hakuna kitu kama hicho maana ningepewa tu habari au hata ningepigiwa simu, hao watu watakuwa wanasambaza tu habari ya uongo,” alisema Wema.


EmoticonEmoticon