Ridhiwani Kikwete Atoa Povu Sakata la Watu Kutekwa na Kupotezwa

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ameitaka Serikali kutokaa kimya na kutoa maelezo ya matukio yanayotokea nchini ili kuondoa wasiwasi na hali ya sintofahamu kwa wananchi.

Ridhiwani amesema hayo jana Bungeni, Mjini Dodoma wakati akichangia mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na bajeti ya ofisi ya Waziri mkuu kwa mwaka 2017/2017.

Ameitaka Serikali akiwemo Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi,  Mwigulu Nchemba kutokalia kimya matukio ya utekaji yanayoendelea nchini.





EmoticonEmoticon