Msanii wa 'HipHop' Bongo Mwana FA amefunguka na kusema kundi la East Coast Team halitaweza kurudi tena katika mambo ya muziki tofauti na taarifa za awali za kurejea upya kwa kundi hilo.
FA ameuweka wazi ukweli huo akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio kwa kusema itakuwa vigumu kurudisha kundi hilo tena katika ulingo wa muziki lakini wanachoweza kipindi hiki ni kufanya 'collabo' ambayo itakuwa inawakutanisha pamoja yeye GK na AY.
"Tulifanya ngoma mbili tatu ila hatukukubaliana kuziachia pia East Coast haiwezi kurudi kwa pamoja lakini mimi, GK na AY tunaweza kufanya kazi kwa pamoja kwani ni jambo rahisi". Alisema FA
Pamoja na hayo msanii huyo amesema tayari amesharekodi kazi nyingi amezihifadhi maktaba kwake kwa kuwa anaogopa kuzitoa katika kipindi hiki.
Nina kazi nyingi katika maktaba nasubiria 'timing' tu niachie maana sasa hivi kuna mambo mengi yanaendelea unaweza ukatoa wimbo hamna mtu anayesikiliza, watu wanaweka bando kufuatilia ubuyu tu, kwahiyo acha patulie kidogo tutaangusha" Alisema FA
EmoticonEmoticon